Moyo lyrics

by

Diamond Platnumz


[Verse 1]
Pole, pole, pole, pole
Pole, pole moyo wangu
Masikini pole
Pole mtima wangu
Haikuwa dhamira
Haikuwa kusudi langu
Haikuwa dhumuni waala
Haikuwa malengo yangu
Ila tuseme labda moyo
Pengine sio ridhiki
Maana nimejitahidi sana
Malengo hayafiki
Kama kuswali naswali sana
Mpaka sunna za usiku
Kazi nimetafuta saana
Ila siambulii kitu
Staki kukufuru Mungu
Sababu najua ni mapito
Japo, inakatisha tamaa
Ila siku yangu ipoo

[Chorus]
Moyo (usiumiee)
Moyo wangu (ni mapito)
Ooh moyo (haya yote mitihani na yana mwisho)
Moyo wangu moyo (usiumie)
Moyo (ni mapito)
Ooooh moyo (haya yote mitihani na yana mwisho)
[Verse 2]
Penzi maua
Pesa mbolea
Hata shemeji yako ana
Mengi ila, hawezi ongea
Moyo
Najitahidi jiepusha vya watu
Ni majaribu aah
Japo nna shida ila naepuka tamaa
Moyo, nlitamani siku moja
Na mimi nimjengee mama
Ila ndo vile tu umasikini
Mipango inakwama
Hua naumia watoto shuleni
Wakifukuzwa ada
Najiona mjinga
Yani sio bora baba
Staki kukufuru Mungu
Najua ni mapito
Maana riziki mafungo
Nami langu siku lipo

[Chorus]
Moyo (usiumiee)
Moyo wangu (ni mapito)
Ooh moyo (haya yote mitihani na yana mwisho)
Moyo wangu moyo (usiumie)
Moyo (ni mapito)
Ooooh moyo (haya yote mitihani na yana mwisho)
[Outro]
Moyo
Moyo
A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #
Copyright © 2012 - 2021 BeeLyrics.Net